Waendesha mashitaka kwenye kesi za jinai za Trump wafutwa
28 Januari 2025Matangazo
Maafisa hao wamesema hawawezi kuwaamini waendesha mashitaka hao. Wafanyikazi hao walifanya kazi katika uchunguzi wa mwanasheria maalum Jack Smith uliosababisha kufunguliwa mashitaka ambayo sasa yametupiliwa mbali dhidi ya Trump.
Hatua hiyo imewaathiri karibu waendesha mashtaka kumi ambao walikuwa kwenye kesi ya namna Trump alizishughulikia nyaraka za siri na kesi yake ya kuingilia uchaguzi. Mwanasheria maalum Jack Smith aliamua bila upendeleo kuzitupilia mbali kesi zote mbili dhidi ya Trump muda mfupi baada ya uchaguzi wa Desemba, akitaja sera ya Wizara ya Sheria inayokataza kumshtaki rais aliye madarakani. Alijiuzulu kutoka kwa wadhifa wake mwishoni mwa muhula wa urais wa Biden.