Wimbi la pili la uvamizi wa nzige wa jangwani linahofiwa kusababisha athari kali kwa usalama wa chakula, nzige hao wanapoendelea kushuhudiwa maeneo ya kaskazini na kati mwa Kenya. Serikali ya nchini hiyo inakiri kukabiliwa na changamoto katika kuibali hali, ikihimiza matumizi ya vifaa vya kidigitali pamoja na mafunzo ya kunyunyizia dawa.