WIESBADEN: Mshukiwa wa pili asakwa na Ujerumani
23 Agosti 2006Polisi nchini Ujerumani wamesema mtuhumiwa wa pili kuhusika na njama iliyoshindwa kuripua mabomu katika treni mbili za abiria,huenda ikawa ameondoka Ujerumani na anajaribu kukimbilia Lebanon.Mkuu wa idara inayoshughulikia uhalifu nchini Ujerumani,Joerg Ziercke amesema,juhudi za kutaka kumkamata mtuhumiwa huyo zimeimarishwa nchini Ujerumani na nchi za ngámbo.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ujerumani,mshukiwa huyo ni M-Lebanon mwenye umri wa miaka 20 na anaitwa Jihad Hamad.Inasemekana kuwa aliishi Cologne. Mshukiwa mwingine aliekamatwa Kiel kaskazini mwa Ujerumani,siku ya Jumamosi ni mwanafunzi wa Ki-Lebanon,Yusuf Mohammed alie na miaka 21.Waendesha mashtaka wamesema,taarifa waliopewa na idara ya upelelezi ya jeshi la Lebanon imesaidia kumkamata mtuhumiwa huyo kabla ya kutoroka Ujerumani.