WHO yahimiza kuhusu makubaliano ya kuzuia majanga
22 Februari 2025Ghebreyesus amesema hayo jana wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya kutafuta makubaliano hayo kabla ya wiki ya mwisho ya mjadala katika makao makuu ya WHO mjini Geneva, huku kukiwa na hatua kidogo za maendeleo zilizopigwa.
Ghebreyesus ameongeza kuwa mataifa yalikuwa yamefikia kilele cha kuhitimisha makubaliano hayo ya kihistoria ya kukabiliana na majanga ya siku zijazo kwa pamoja.
Mazungumzo ya mkataba wa kushughulikia majanga yaanza tena
Kiongozi huyo wa WHO amesema kumekuwa na hatua za maendeleo labda sio kwa kiwango kilichotarajiwa lakini akaongeza kuwa kuna matumaini.
Pia amewaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba wako katika hatua muhimu wanapoelekea kukamilisha makubaliano ya majanga kabla ya kongamano la kila mwaka la maamuzi laWHO litakalofanyika mwezi Mei.