AfyaUganda
WHO yaipongeza Uganda kutoa chanjo ya majaribio ya Ebola
8 Februari 2025Matangazo
Mike Ryan, ametoa pongezi hizo alipozungumza na shirika la habari la AFP alipoitembelea Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda iliyopo mjini Entebbe.
Soma pia: Uganda yaanzisha chanjo ya majaribio ya kuzuia Ebola
Kifo cha nesi mmoja wiki iliyopita kiliashiria mlipuko wa sita wa Ebola nchini Uganda, aina ya virusi vya Sudan ambayo hadi sasa aina chanjo iliyoidhinishwa. Kati ya aina tano za virusi vya Ebola, moja tu ndiyo yenye chanjo iliyoidhinishwa rasmi.