WHO yakaribisha tangazo la kumalizika Marburg Tanzania
13 Machi 2025Matangazo
Shirika hilo limesema leo kwamba ushirikiano wa karibu na nchi hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa katika kupatikana matokeo hayo.
Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X shirika la WHO tawi la kanda ya Afrika, limeeleza kwamba ushirikiano na mamlaka ya Tanzania, usaidizi wa WHO na washirika wake pamoja na kujitolea kwa timu zilizokuwa mstari wa mbele, ndiyo mambo yaliyofanikisha juhudi za kuwalinda raia na kuzuia kusambaa ugonjwa huo.