WHO: Vifo 60 DRC huenda vilisababishwa na maji kuchafuliwa
1 Machi 2025Hata hivyo, maafisa hao hawakutoa hitimisho la uhakika huku Mkuu wa kitengo cha dharura wa WHO Dokta Michael Ryan akisema bila kutoa pia maelezo zaidi kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa tukio la vifo katika moja ya kijiji linahusishwa na chanzo cha maji kuchafuliwa na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.
Ugonjwa usiojulikana uilirikodiwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu katika kijiji cha Boloko, ambapo inaarifiwa watoto watatu walikufa baada ya kula nyama ya popo na baadaye katika kijiji cha Bomate huko Basankusu.
Soma pia:Ugonjwa usiojulikana waua zaidi ya watu 50 nchini Kongo
Dalili za ugonjwa huo ni homa, mafua, kukohoa, kutokwa damu puani, matatizo ya misuli, kuhara na kutapika. Tatizo hilo la kiafya liliibua hofu miongoni mwa raia ambao baadhi walilazimika kuyahama makazi yao wakihofia kuambukizwa.