WHO kujadili kupunguza bajeti baada ya Marekani kujitoa
3 Februari 2025Matangazo
Nyaraka zilizotolewa leo na WHO kuelekea kikao chake cha kila mwaka cha bodi ya utendaji zinaonesha, shirika hilo linapanga kupunguza fedha za kugharamia miradi kutoka dola bilioni 5.3 hado bilioni 4.9.
Kiwango hicho ni sehemu ya mapendekezo ya bajeti ya WHO kwa mwaka 2026/2027 ya kiasi dola bilioni 7.5 inayojumuisha miradi ya kutokomeza ugonjwa wa polio na dharura nyingine za kiafya. Marekani ni mchangiaji mkubwa zaidi miongoni mwa nchi wanachama wa WHO na uamuzi wa Trump wa kuitoa kutoka shirika hilo ulitarajiwa kuwa athari za kibajeti.
Soma pia:Umoja wa Afrika 'wasikitishwa' na Marekani kujiondoa WHO
Kwenye mkutano ulianza leo, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameurai utawala wa Trump kutafakari tena uamuzi huo.