Janga
WFP yadondosha chakula kwa maelfu ya watu Sudan Kusini
7 Julai 2025Matangazo
Mgogoro wa Sudan Kusini umesababisha baadhi ya jamii kukabiliwa na hatari ya baa la njaa.
Kulingana na taarifa ya WFP, usambazaji huo wa chakula ni wa kwanza kufanywa na shirika hilo ndani ya miezi minne katika kaunti za Nasir na Ulang zinazoweza kufikiwa kupitia njia hiyo ya anga pekee.
Sudan Kusini imekuwa katika migogoro ya mara kwa mara tangu rais Salva Kiir alipotofautiana na makamu wake wa zamani Riek Machar na kusababisha uhasama wa wazi mwezi Machi.
Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya maafa huko Sudan
Hali hiyo imezua hofu ya kurejea vita kamili katika taifa hilo changa duniani ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe tayari vimekwisha sababisha mauaji ya watu lakini 400,000 kati ya mwaka 2013 na 2018