WFP kusitisha msaada kwa wanawake na watoto 650,000 Ethiopia
22 Aprili 2025Shirikala WFP limeonya kuwa kundi hilo la wanawake na watoto litakuwa miongoni mwa watu milioni 3.6 nchini Ethiopia ambao hawataweza tena kupata msaada wa chakula katika wiki zijazo bila ufadhili mpya wa dharura.
Shirika la WFP larejesha msaada wa chakula Ethiopia
Katika taarifa yake, WFP imesema inalazimika kusitisha matibabu kwa wanawake hao na watoto mwezi Mei kutokana na uhaba huo wa fedha na kuongeza kwamba ilikuwa imepanga kuwafikia akina mama na watoto milioni mbili kwa msaada wa lishe ya kuokoa maisha mwaka huu wa 2025.
Mkurugenzi wa WFP nchini Ethiopia Zlatan Milisic, ameliambia shirika la habari la AFP anadhani ni wakati muhimu kuukumbusha ulimwengu na wafadhili wao wengine kwamba hali ya kibinadamu nchini humo sio nzuri sana, na kwamba itazidi kuwa mbaya.