WELLINGTON : Polisi yamaliza mzozo wa bomu
16 Septemba 2005Katika mkesha wa uchaguzi mkuu wa New Zealand polisi imemkamata mwanaume mmoja aliyetishia kujiripuwa venginevyo apewe nafasi ya kuzungumza na Waziri Mkuu Helen Clark.
Polisi ilivamia hoteli aliyokuwako mtu huyo baada ya mvutano wa masaa 13 ambao ulisababisha kuhamishwa kwa maelfu ya watu kutoka katika mji wa kaskazini wa Tauranga.Polisi imesema imegunduwa bomu bandia.
Wakati huo huo uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwepo kwa mchuano mkali katika uchaguzi huo kuwahi kushuhudiwa katika historia ya taifa hilo la Pasifiki.Suala la New Zealand kupiga marufuku silaha za nuklea na mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea limekuja kuwa mada muhimu katika uchaguzi huo.
Kiongozi mkuu wa upinzani Dan Brash amesema yuko tayari kufutilia mbali sera ya kupiga vita silaha za nuklea iwapo nchi hiyo itakuwa na mkataba huru wa biashara na Marekani.
Waziri Mkuu wa chama cha Labour Helen Klark amelishutumu wazo hilo.