WEIMAR: Siku ya ukombozi wa kambi ya Buchenwald
10 Aprili 2005Wanasiasa mashuhuri wa Ujerumani hii leo walikusanyika katika mji wa Weimar,mashariki mwa nchi kuadhimisha mwaka wa 60 tangu kukombolewa kwa kambi ya Buchenwald.Tarehe 11 April mwaka 1945,Buchenwald ilikuwa kambi ya kwanza ya Manazi kukombolewa na majeshi shirika.Kiasi ya wafungwa 21,000 walinusurika,lakini zaidi ya 56,000 waliuawa katika kambi hiyo kati ya mwaka 1937 na 1945.Hii leo Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani alikuwa kiongozi wa kwanza kuwahotubia kiasi ya wageni 1,000 kutoka nchi 26 mbali mbili.Miongoni mwa wageni hao ni kama watu 500 waliookolewa kutoka kambi ya Buchenwald na wanajeshi 50 wa zamani wa Kimarekani waliosaidia kuikomboa kambi hiyo.Kansela Schroeder katika hotuba yake amesema,viongozi wanaoiwakilisha Ujerumani ya hii leo yenye udemokrasia watahakikisha kuwa udhalimu,utumiaji wa nguvu, ubaguzi wa kikabila na Wayahudi hautopata nafasi ya kujichomoza.