Uingereza yaombwa kuchunguza kifo cha ''Agnes Wanjiru''
7 Aprili 2025Waziri wa ulinzi wa Uingereza John Healey amekutana leo na familia ya mwanamke mmoja aliyekutwa amefariki baada ya kuonekana mara ya mwisho akiwa na mwanajeshi mmoja wa Uingereza, mnamo mwaka 2012.
Waziri huyo wa ulinzi wa Uingereza aliweka wazi kwamba amedhamiria kuona mwafaka unapatikana juu ya kesi hiyo ambayo haijapatiwa ufumbuzi.
Kisa hicho kilichoangaziwa sana,kilisababisha mshtuko nchini Kenya huku familia ya Agnes Wanjiru, kwa muda mrefu ikiiomba serikali ya Uingereza kuanzisha uchunguzi kamili kuhusu kifo hicho. soma pia: Kenya yafanya mikutano ya hadhara kuhusu madai ya dhuluma na wanajeshi wa Uingereza
Mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21 alikutwa kwenye chemba ya maji taka akiwa amekufa,baada ya kudaiwa alikwenda kupata burudani na mwanajeshi wa Uingereza katika hoteli moja ya mji wa Nanyuki ambako kuna kambi ya jeshi la Uingereza.
Waziri Healey atakutana pia na rais William Ruto baadae leo.