MigogoroMashariki ya Kati
Israel kuidhinisha mipango ya kuidhibiti Gaza City
18 Agosti 2025Matangazo
Hayo ni kulingana na ripoti iliyochapishwa kwenye tovuti ya habari ya Walla ya Israel. Ripoti hiyo imebainisha kuwa wanajeshi takriban 80,000 watapelekwa kuudhibiti mji huo kwa mujibu wa mipango ya mkuu wa utumishi wa Israel, Eyal Zamir.
Ripoti ya tovuti hiyo imeongeza kuwa jeshi la Israel linatazamiwa kuuzingira mji huo na kuisambaratisha miundombinu ya Hamas iliyosalia pamoja na alama muhimu zilizosalia za utawala wa kundi hilo.
Hayo yanaendelea wakati wasuluhishi wakiendelea na juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita na kuwaachilia mateka kwenye mzozo huo uliodumu kwa karibu miaka miwili sasa.