Serikali ya Israel yamtaka Mkuu wa Majeshi kutekeleza amri
6 Agosti 2025Matangazo
Katz ameitoa kauli hiyo baada ya ripoti katika vyombo vya habari vya Israel kueleza kwamba mkuu wa majeshi anapinga mpango wa serikali wa kuikalia kikamilifu Gaza akisema utakuwa "mtego".
Vyombo hivyo vimeripoti pia kuwa Netanyahu atakutana hivi leo na baraza lake la usalama ili kuchukua uamuzi wa mwisho kuhusu hatua zinazofuata katika vita hivyo kwenye ardhi ya Palestina. Tarifa zinaeleza kuwa jeshi la Israel linatarajiwa kutanua operesheni zake katika eneo lote la Gaza , ikiwa ni pamoja na maeneo yenye watu wengi ambako mateka wanaaminika kushikiliwa.