Waziri wa Ulinzi Struck aona ikihatarika Afghanistan
14 Desemba 2003Matangazo
BERLIN: Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck anakhofia yatafanyika mashambulio ya kigaidi kutokana na kufanyika mkutano wa Baraza Kuu la Bunge nchini Afghanistan. Makundi mbali mbali kama vile Taliban na Al Qaida yanajaribu kurejea madarakani nchini alisema Waziri huyo wa Mambo ya Ulinzi wa Ujerumani.