Waziri wa sheria DRC aandamwa kwa ufisadi
22 Mei 2025Matangazo
Spika wa bunge katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoVital Kamerhe amesema, waziri wa sheria Constant Mutamba, atahojiwa na tume maalum ya bunge kuhusu tuhuma za kusimamia matumizi mabaya ya takriban dola milioni 20 zilizokusudiwa kutumika kulipa fidia za walioathirika na vita.
Kamerhe, jana alisema bunge la taifa litatangaza orodha ya wabunge watakaounda tume hiyo maalum ya kumuhoji waziri huyo wa sheria kabla ya kupigwa kura itakayoamuwa ikiwa anapaswa kufunguliwa mashtaka au la.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali,aliliandikia barua bunge iliyosomwa jana akilitaka kupiga kura kumuondolea kinga ya ubunge, waziri Mutamba, ili achunguzwe kuhusu tuhuma hizo za ufisadi.