Waziri wa mambo ya nchi za nje wa ujerumani atunukiwa tunzo ya Leo Baeck
11 Mei 2005Matangazo
Halmashauri kuu ya wayahudi nchini Ujerumani imemtunukia waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer zawadi ya Leo-Baeck .Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Paul Spiegel amesifu juhudi za upatanishi za waziri Fischer katika mzozo wa mashariki ya kati.Katika ahotuba yake waziri wa mambo ya nchi za nje Joscvhka Fischer amesema „maisha ya sasa ya wayahudi nchini Ujerumani ni ushindi muhimu dhidi ya wanazi.“ Zawadi ya Leo Baeck ni ya fahari kabisa miongoni mwa zawadi zinazotolewa na halmashauri kuu ya wayahudi nchini Ujerumani.Zawadi hiyo imepewa jina la Rabin wa jiji la Berlin Leo Beck.