Ujerumani yasema msaada zaidi unahitajika Ukanda wa Gaza
22 Agosti 2025Hii ni baada ya ripoti ya tathmini ya Usalama wa upatikanaji wa Chakula, IPC, kutangaza baa la njaa katika ukanda huo.
Radovan amesema ripoti hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, inaonesha namna eneo hilo linavyopitia hali ngumu ya kibinaadamu.
Baa hilo la njaa kwa kawaida huwa linatangazwa rasmi wakati vigezo fulani vinapopitishwa ikiwemo, asilimia 20 ya jamii kukabiliwa na upungufu wa chakula, asilimia 30 ya watoto kukumbwa na utapiamlo na angalau watu wazima wawili na watoto wanne kati ya watu 10,000 kupoteza maisha kila siku kutokana na njaa au magonjwa yanayotokana na utapia mlo, matukio ambayo yote yameshashuhudiwa Gaza.
Hata hivyo ripoti hiyo imesema ufikiaji wa malori ya misaada imeimarika japo ikasisitiza kuwa bado msaada zaidi unahitajika haraka katika eneo hilo.