UchumiUlaya
EU inahitaji hatua madhubuti kukabili ushuru wa Marekani
13 Julai 2025Matangazo
Klingbeil ameyasema hayo Jumapili 13.07.2025 katika mahojiano na gazeti la Sueddeutsche la Ujerumani. Ameongeza kuwa ushuru huo hauna mshindi na unatishia uchumi wa Marekani na biashara za Ulaya.
Waziri huyo wa Fedha wa Ujerumani ametoa pendekezo hilo siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa bidhaa za Umoja wa Ulaya na Mexico zinazoingia Marekani zitatozwa ushuru wa asilimia 30 kuanzia Agosti Mosi mwaka huu.
Kwa upande wake Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von Der Leyen amesema umoja huo utaendelea kuvuta muda wa kulipa kisasi kwa ushuru wa Marekani hadi Agosti, wakati wakitafuta makubaliano ya kuzuia ushuru huo mkubwa wa asilimia 30.