MigogoroMashariki ya Kati
Waziri wa Fedha wa Israel: "Gaza itaangamizwa kabisa"
6 Mei 2025Matangazo
Mwanasiasa huyo mwenye siasa kali za mrengo wa kulia ameyasema hayo katika mkutano uliokuwa ukijadili suala la makaazi ya walowezi wa kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Kauli ya kiongozi huyo imetolewa wakati jumuiya ya kimataifa ikikosoa hatua iliyoidhinishwa jana na serikali ya Israel ya kulitwaa eneo zima la Ukanda wa Gaza na kuendelea kulishikilia kwa muda usiojulikana.
Hayo yakiarifiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu OCHA limethadharisha kuwa hali inazidi kuwa mbaya katika ardhi ya Palestina iliyoharibiwa na vita baada ya takriban wiki tisa za mzingiro kamili wa Israel.