MigogoroSudan
Hamdok: Ushindi wa jeshi la Sudan hauwezi kuvimaliza vita
5 Juni 2025Matangazo
Abdalla Hamdok amesema ushindi wake wa hivi karibuni wa kutwaa tena mji mkuu Khartoum na maeneo mengine hautamaliza vita vilivyodumu kwa miaka miwili nchini humo.
Katika mahojiano ya nadra na shirika la habari la AP, Hamdok amesema hakuna ushindi wa kijeshi, huko Khartoum au kwingineko, unaoweza kuvimaliza vita hivyo.
Amesema hayo pembezoni mwa kongamano la utawala bora la Wakfu wa Mo Ibrahim nchini Morocco na kuongeza kuwa haiwezakani kufikiwa suluhu kijeshi na hakutakuwa na upande utakaopata ushindi wa moja kwa moja.
Amesisitiza kwama jaribio lolote la kuunda serikali nchini Sudan kwa wakati huu halitakuwa na maana na kuongeza kuwa amani ya kudumu haitapatikana kama mzizi wa mzozo hautashughulikiwa kwanza.