SiasaIsrael
Naftali Bennett amtaka Netanyahu kuondoka madarakani
29 Juni 2025Matangazo
Bennett hata hivyo amekataa kuweka wazi ikiwa ana nia ya kupambana naye kwenye uchaguzi ujao. Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Israel amesema Netanyahu amekuwa madarakani kwa miaka 20 akiitaja kuwa mingi mno huku akimtuhumu kiongozi huyo kuwa na jukumu kubwa kwa migawanyiko inayoshuhudiwa kwenye jamii ya Israel.
Bennett amesisitiza kuwa upinzani umekuwa pia ukimtaka Benjamin Netanyahu kuondoka hasa kutokana na alivyoshughulikia vita vya Gaza. Kwa sasa, hakuna uchaguzi wowote uliyopangwa kufanyika kabla ya mwishoni mwa mwaka 2026, lakini kuitishwa uchaguzi wa mapaema ni jambo la kawaida katika siasa za Israel.