Utawala wa sheriaGuinea
Waziri mkuu wa zamani Guinea Conakry ahukumiwa miaka 5 jela
28 Februari 2025Matangazo
Ibrahima Kassory Fofana aliyewahi kuwa waziri mkuu chini ya serikali ya rais Alpha Conde,pia alitozwa faini ya faranga bilioni 2 ambazo ni sawa na dola laki (230,000) na mahakama hiyo mjini Conakry.
Fofana amekutwa na hatia ya kutumia vibaya fedha za umma faranga bilioni 15 ambazo zilitengwa kwaajili ya miradi ya shughuli za ustawi wa jamii, ikiwemo wakati wa janga la Corona,katika serikali iliyopita.
Waziri mkuu huyo wa zamani Guinea ni mmoja kati ya maafisa wengi wa serikali hiyo iliyoondolewa madarakani,kushtakiwa na kuhukumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi na makosa mengine ya uporaji fedha katika mahakama maalum iliyoundwa baada ya utawala wa kijeshi nchini humo kutwaa madaraka.