Waziri Mkuu wa Uingereza abadilisha baraza lake la mawaziri
6 Septemba 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amemteua naibu wake mpya na mawaziri wa Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani katika mabadiliko makubwa yanayonuia kurejesha mamlaka yake baada ya Naibu Waziri Mkuu Angela Rayner kujiuzulu kutokana na makosa ya kulipa ushuru mdogo wa mali zake.
Katika mabadiliko hayo waziri wa mambo ya nje David Lammy, sasa ndiye naibu waziri mkuu mpya na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Yvette Cooper.
Aliyekuwa Waziri wa Sheria, Shabana Mahmood, sasa ndiye Waziri mpya wa Mambo ya Ndani. Vyanzo ndani katika ofisi ya Keir Starmer vimeeleza kuwa serikali ya Uingereza sasa imepata nguvu tena kutokana na mabadiliko hayo.