Waziri mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou aondolewa
9 Septemba 2025Matangazo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo atakubali kujiuzulu kwa waziri mkuu Francois Bayrou baada ya serikali yake kukataliwa katika kura ya imani.
Macron yuko mbioni kutafuta waziri mkuu wa saba kujaza pengo lililojitokeza kuepusha mgogoro mpya wa kisiasa Ufaransa baada ya hapo jana Bayrou kupoteza kura ya imani aliyoiitisha yeye mwenyewe.
Matokeo ya kura iliyopigwa jana katika bunge la kitaifa, yanaonesha wabunge 364 walipiga kura kusema hawana imani na serikali huku 194 pekee wakisema wana imani nayo.
Macron atakutana na Bayrou leo Jumanne "kukubali kujiuzulu kwa serikali yake.