Waziri Mkuu wa Thailand asimamishwa kazi
1 Julai 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra amesimamishwa wakati ambapo mabadiliko yamefanyika katika baraza la mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Paetongtarn alijikabidhi wadhifa wa waziri wa utamaduni, na kwa maana hiyo huenda akaendelea kuwa na madaraka na kubaki katika uongozi.
Hata hivyo, nafasi yake na muungano wake umedhoofishwa kwa kiwango kikubwa, japokuwa bado una idadi kubwa ya wabunge katika bunge, hali inayopunguza uwezekano wa kuitishwa uchaguzi wa mapema.
Mustakbali wa Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra haufahamiki kwa kuwa hakuna muda uliowekwa kwa mahakama ya katiba kukamilisha uchunguzi wake, lakini mahakama ikibaini amekiuka maadili huenda akaondolewa kabisa ofisini.