SiasaAsia
Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba ajiuzulu
7 Septemba 2025Matangazo
Ishiba, aliyekuwa madarakani tangu Oktoba mwaka jana, alikabiliwa na ukosoaji unaoongezeka na wito wa kuachia ngazi ndani ya chama chake cha Liberal Democratic Party (LDP) kufuatia kupoteza wingi wa viti bungeni.
Amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake hadi kiongozi mpya wa chama atakapochaguliwa, akisisitiza kuwa "sasa ndiyo wakati sahihi wa kujiuzulu.”
Tangazo lake limekuja muda mfupi baada ya kukamilika kwa makubaliano ya kibiashara na Marekani. Ushirika wa LDP na chama kidogo Komeito ulipoteza wingi wa viti katika baraza la juu mwezi Julai, baada ya awali kupoteza wingi wake katika baraza la chini Oktoba. Tangu wakati huo serikali ya Ishiba imekuwa ikifanya kazi kama serikali ya wachache.