Waziri Mkuu wa Japan aapa kubaki madarakani
21 Julai 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba ameapa kuendelea kubaki madarakani huku mazungumzo muhimu ya biashara na Marekani yakikaribia.
Kauli hiyo ameitoa baada ya muungano wake unaotawala kushindwa kupata wingi wa kutosha katika uchaguzi wa bunge lenye viti 248 uliofanyika jana Jumapili.
Chama cha Liberal Democratic LDP ambacho tayari kilikuwa na idadi ndogo ya wabunge katika baraza la wawakilishi tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita, kilikabiliwa na ongezeko la raia kutoridhika nacho kuhusiana na mfumuko wa bei, kashfa za rushwa na ongezeko la kauli za kupinga uhamiaji.
Ishiba amesema ataendelea na wadhifa wake ili kuiongoza Japan kupata mkataba wa kibiashara na Marekani kabla kuwekewa ushuru.