Waziri Mkuu wa Japan aamua kujiuzulu
7 Septemba 2025Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa Ishiba, mwenye umri wa miaka 68, anataka kuepusha mgawanyiko wa chama, huku shinikizo la kuachia madaraka likiongezeka kutoka kwa viongozi wakuu akiwemo waziri mkuu wa zamani Taro Aso ambaye anasalia kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama.
Uchaguzimpya wa uongozi unaweza kuitishwa wiki hii, ingawa kipindi chake kilikuwa kimalizike 2027. Mpinzani wake mkuu, Sanae Takaichi, mwenye msimamo mkali wa kizalendo, tayari ameashiria kuwania wadhifa huo.
LDP, ambayo imeongoza Japan karibu bila kupumzika tangu mwaka 1955, inakabiliwa na upinzani kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa hasa mchele, kushuka kwa viwango vya maisha, na kashfa za ufisadi.
Ishiba alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama mwaka jana katika jaribio lake la tano, akiapa kuijenga "Japan mpya''.